Tanzania kuna "web developers" wengi sana. Wengine ni wazuri kweli. Wengine wanachukua pesa yako na kukuacha na website inayofanana na kila mtu. Na wengine wanaanza vizuri lakini wanaisha support baada ya wiki mbili.
Makala hii itakusaidia kuchagua vizuri bila kutegemea luck.
Angalia Portfolio Kwanza Kabla ya Mazungumzo Mengine
Hii ndiyo test ya kwanza na muhimu zaidi. Mtengenezaji mzuri ana portfolio ya real work sio designs za Canva au mockups tu, bali websites za live ambazo unaweza kutembelea.
Unapoona portfolio, angalia hivi:
- Je, sites zinafunguka vizuri kwenye simu yako? mobile test ya haraka
- Je, zinapakia haraka? bonyeza stopwatch. Zaidi ya sekunde 4 ni tatizo
- Je, design inaonekana ya mwaka huu au ya 2015?
- Je, kuna variety? kama sites zote zinaonekana sawa, wana template moja wanayotumia kwa wote
Na kama wanasema "haziko online bado" au "client hakutaka itionekane" hiyo ni red flag. Kazi nzuri huwezi kuificha.
Maswali 6 ya Lazima Kuuliza Kabla ya Kulipa
- "Je, nitamiliki code yote ya website baada ya kukabidhi?"
Jibu sahihi: "Ndiyo, kabisa." Ukisikia "utapata access ya admin tu" acha. Unachokipa pesa ni kazi yako inabidi iwe yako kamili. - "SEO ya msingi imejumuishwa?"
Wengi wanasema "ndiyo" lakini hawafanyi zaidi ya title tag moja. Maswali ya follow-up: "Je, sitemap inaundwa? Google Search Console inasanidiwa? Schema markup ipo?" Kama hawajui maswali haya, hawajui SEO. - "Hosting na domain nimejumuishwa?"
Wengi wanakucharji kwa website, kisha unagundua hosting unailipa wewe na hawakuambia. Bei kamili ni yote pamoja. Kama la, hakikisha unajua exactly utalipa kiasi gani kwa mwaka. - "Support baada ya launch ni nini hasa?"
"Support" inaweza kumaanisha chochote. Uliza specifically: "Kama website inabreak baada ya miezi 2, mnafanya nini? Kuna gharama?" Weka hii maandishwa kwenye agreement. - "Muda wa kukamilisha ni ngapi guaranteed?"
Sio estimate guaranteed. Na ni nini kitatokea kama hawafiki deadline? Fanya hii iwe sehemu ya contract. - "Mnaweza kunionyesha examples za clients wanaofanana na biashara yangu?"
Web designer wa hospitali na web designer wa boutique ni skills tofauti. Mtu aliyefanya websites za service businesses anajua challenge za service businesses.
Mazungumzo ya awali (consultation) ni fursa yako ya kujua exactly unayopata usikimbie hapa.
Red Flags Simama Unapoona Hizi
- 🚩 Bei ya TZS 50,000100,000 kwa "website kamili" hii ni template ya cheap au kazi ya amateur
- 🚩 Hawana portfolio yoyote au portfolio ni ya designs tu, sio live websites
- 🚩 Wanakuomba 100% ya pesa mapema
- 🚩 Hawatoi quotation ya maandishi verbal quotes hazilindiwi
- 🚩 Wanasema "itakuwa tayari wiki ijayo" bila kujua scope yako hii inaonyesha hawatafikiria kazi halisi
- 🚩 Hawajui SEO ni nini website bila SEO ni kama duka bila signboard
Ukweli wa kusikitisha: Wafanyabiashara wengi Tanzania wamepoteza TZS 200,000500,000 kwa developers ambao walitoa website ya template na kutoweka. Mwaka baadaye wanakuja kwetu ku-rebuild tangu mwanzo. Chagua vizuri mara ya kwanza.
Vigezo 5 vya Mtengenezaji Mzuri
| Kigezo | Unavyopima |
|---|---|
| Portfolio ya Live Sites | Angalia kwenye simu yako moja kwa moja |
| SEO Knowledge | Waulize kuhusu meta tags, schema, sitemap wajua? |
| Communication | Wanajibu WhatsApp ndani ya masaa 24? Professional? |
| Quotation ya Maandishi | Detailed, itemized, na deadline |
| Contract/Agreement | Scope, timeline, payment structure, ownership ya code |
Kama tayari una website na unashangaa kama inahitaji kubadilishwa, angalia dalili 7 zinazoonyesha website yako inahitaji redesign.
Na kama unataka kujua ni kiasi gani cha pesa unachopaswa kutumia, soma bei halisi za kutengeneza website Tanzania.
Maswali Yanayoulizwa
Kila moja ina pros na cons. Freelancer mzuri bei nafuu, communication direct, flexible. Tatizo: ukienda ugonjwa au safari, kazi inasimama. Agency team, backup, na process iliyowekwa. Inaweza kuwa expensive zaidi. Kwa biashara ndogo hadi ya kati, freelancer au boutique agency (kama sisi) mara nyingi ni best value. Kitu cha muhimu zaidi kuliko label ni: wana portfolio ya live work, wanajibu maswali yako vizuri, na wana process wazi.
Ndiyo, inawezekana. Lakini zingatia: mtengenezaji wa nje anaweza kushindwa kuelewa specifics za Tanzania M-Pesa integration, local SEO, Kiswahili content, na culture ya wateja wa Tanzania. Mtengenezaji wa ndani au anayejua Tanzania vizuri ana advantage kubwa katika hizi areas.
Absolutely daima. Hata kwa mtengenezaji unayemjua personally. Agreement inabainisha: scope ya kazi, timeline, payment structure, ownership ya code, na support period. Hii inalinda pande zote mbili. Mtengenezaji anayekataa kuandika agreement hiyo ni red flag kubwa sana.
Gadaki ni Choice Yako Nzuri Tanzania
Portfolio halisi. Bei wazi. SEO ya msingi kwenye kila website. Wasiliana nasi leo jibu ndani ya masaa 24.
Comments
Loading comments
Leave a Comment
Your email address will not be published. All comments are moderated before appearing.